Kutoa misaada kwa zaidi ya familia (300) za mashahidi na wenye kipato duni

Maoni katika picha
Mawakibu za kutoa misaada zilizopo Bagdad Karakh ambazo zipo chini ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya zimetoa misaada kwa zaidi ya familia (300) za mashahidi na watu wenye kipato duni katika mkoa wa Najafu Ashrafu, ikiwa ni sehemu ya harakati zao za kibinaadamu.

Kuhusu misaada hiyo tumeongea na bwana Haidari Sudani ambae ni kiongozi katika harakati hizo, amesema kua: “Harakati hii ni sehemu ya harakati zilizo kuhusisha mikoa mingi, kwa lengo la kupunguza ugumu wa maisha kwa familia za mashahidi na watu wenye kipato duni, pamoja na kuonyesha umuhimu na utukufu wa familia hizo”.

Akaongeza kua: “Kazi yetu haishii kwenye kuwasaidia wapiganaji wa serikali na Hashdi Shaábi peke yake, pamoja na kwamba hao ndio kipaombele chetu lakini hatuja sahau makundi mengine, baada ya kupata maombi husimama kuyajibu kwa nguvu zote, tumesimama kusaidia mayatima na kujenga upya kila palipo bomolewa na magaidi ili kurudisha furaha kwa wahanga”.

Akabainisha kua: “Bidhaa tunazo gawa ni vyakula vya aina mbalimbali, na vitu vingine vinavyo hitajiwa na familia zikiwemo nguo na vifaa tofauti vya nyumbani, hutembelewa sehemu ya familia hizo na kubaini mahitaji yao kisha hupelekewa misaada kulingana na mahitaji”.

Akasisitiza kua: “Hakika idara ya Bagdad Karakh ipo mstari wa mbele katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu tangu ilipotolewa fatwa takatifu ya jihadi kifaya hadi sasa, kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na wahisani wanao shindana katika mambo ya heri, misafara yetu ya kugawa misaada haijasimama, sawa iwe katika kusaidia mayatima, familia za mashahidi, ujenzi na ukarabati wa shule zilizo bomoka wakati wa vita sambamba na kusaidia wapiganaji waliopo kwenye uwanja wa mapambano, hatujazuwiliwa na ugumu wa mazingira ya hali ya hewa, sawa kuwe na baridi kali, joto, mvua au vimbunga, kadri umbali unavyo kua mkubwa ndivyo watu wa kujitolea wanavyo ongezeka”.

Akabainisha kua: “Misafara imepewa majina yafuatayo:

  • 1- Msafara wa Ali Akbaru (a.s).
  • 2- Msafara wa Labbaika yaa Hussein (a.s).
  • 3- Maukibu ya Mussa Alkaadhim (a.s)”.

Kumbuka kua idara hii haijaishia kwenye kusaidia familia za mashahidi na mafakiri peke yake, kuna kamati maalum inayo husika na kujenga na kukarabati nyumba za mafakiri na maeneo yanayo tumiwa na Hashdi Shaábi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: