Kutumia njia ya kufundisha kwa masafa ili kujilinda na virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kama sehemu ya kuchukua tahadhari ya virusi vya Korona, Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya tawi la Najafu imeanza kutumia ufundishaji wa njia ya masafa, inatumia mitandao ya mawasiliano katika kufundisha masomo ya Quráni likiwemo somo la hifdhu.

Idara ya Maahadi imesema kua kuna madarasa matano ya kuhifadhi Quráni ambayo bado yanaendelea, kila darasa linawashiriki wengi.

Wakufunzi wanawasiliana moja kwa moja na wanafunzi wao kwa kutumia mtandao wa whatsap, mkufunzi anamsikiliza mwanafunzi moja kwa moja katika sehemu anayotakiwa kusikilizwa, sambamba na kuwapa maelekezo ya matamshi sahihi.

Utaratibu huu umekubalika na kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa washiriki.

Kumbuka kua idara ya Maahadi tukufu inamkakati maalum wa kuendesha masomo ya Quráni na kuhakikisha usalama wa wakufunzi na washiriki, mfumo huu mpya wa usomeshaji ni sehemu ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya korona bila kuacha kutoa elimu ya usomaji wa Quráni kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: