Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) Liwaau/26 Hashdi Shaábi katika mkoa wa Karkuuk kimeitikia wito wa wapiganaji wa Hashdi Shaábi katika wilaya ya Dabsi na Bai Hassan, wa kuwapa stadi za kujilinda na visusi vya Korona na kugawa vifaa vinavyo hitajika katika kujilinda na virusi hivyo.
Msemaji wa kikosi ameongea kua: “Miongoni mwa misafara ya kutoa misaada chini ya maelekezo ya viongozi wa kikosi chetu ya kugawa maski na vipeperushi vya maelekezo ya kiafya kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karkuuk, wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamekwenda katika wilaya ya Dabsi na Bai Hassan kuitikia wito wa vikosi vya wapiganaji wa Hashdi Shaábi katika miji hiyo, na kugawa vitu walivyo hitaji, ambavyo ni maski na vipeperushi vinavyo elekeza namna ya kujilinda na virusi vya Korona”.
Akabainisha kua: “Tumegawa maski na vipeperushi pamoja na misaada mingine kwa vikosi vyote”.
Kumbuka kua wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mji wa Karkuuk walikua wamesha toa mafunzo ya namna ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona katika mkoa huo.