Kitengo cha tarjama kimetoa vitabu kwa lugha ya kiengereza

Maoni katika picha
Kitengo cha tarjama katika kituo cha kimataifa Al-Ameed Lilbuhuthi wa Dirasaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa vitabu kadhaa ilivyo andika moja kwa moja na ilivyo tafsiri kutoka lugha ya kiarabu kwenda kiingereza na kinyume chake.

Kazi hiyo imefanywa na Profesa Haidari Ghazi Mussawi ambae ni rais wa kitengo cha tarjama katika kituo cha kimataifa Al-Ameed Lilbuhuthi, ameandika vitabu vya mada tofauti, mada kuu ikiwa ni (Hussein amebaki na matwaghuti wameondoka), aidha ameandika mfumo wa kikatili uliokuwepo wakati wa utawala wa kidikteta ulio pita na maandamano ya Shaábaniyya.

Vitabu vimesisitiza umuhimu wa kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu ya kuendelea kuwaheshimu maimamu watakasifu pamoja na tawala dhalimu kutaka kufuta haki na kueneza batili, huku vitabu vingine vikiwa vimeandika maelekezo muhimu kutoka kwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani kwa wapiganaji watukufu kwenye uwanja wa vita dhidi ya maadui, sambamba na kuandika misaada iliyo tolewa na Ataba tukufu kwa raia watukufu katika mazingira yote waliyo pitia.

Tambua kua kitengo cha tarjama kipo chini ya kituo cha kimataifa Al-Ameed Lilbuhuthi wa Dirasaat, kitawajibika kutafsiri baadhi ya vitabu kutoka kwenye lugha ya kiarabu kwenda kiengereza na kinyume chake, kwa ajili ya kuweka uhusiano salama kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: