Baada ya miezi miwili: Masayyid watumishi wahitimisha ratiba ya masomo ya Quráni

Maoni katika picha
Idara ya Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ratiba ya masomo ya Quráni, sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) kwa kufanya kikoa cha usomaji wa Quráni tukufu, ratiba iliyokua inalenga kusahihisha na kufundisha usomaji sahihi wa Quráni kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na kundi la waumini mazuwaru watukufu, asubuhi ya leo (8 Rajabu 1441h) sawa na (4 Machi 2020m) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Mimi nakuachieni vizito viwili: kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu, mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu milele). Chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Ataba tukufu na kwa kushirikiana na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, tumefanya ratiba hii ya kufundisha usomaji sahihi wa Quráni na hukumu zake, kwa watu wanaokuja kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ratiba iliyodumu karibu miezi miwili hadi leo tumefika mwisho wa ratiba hiyo, ni matumaini yetu kua tumechangia kueneza utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni na kuwajengea uwelewa zaidi mazuwaru watukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: