Shirika la Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limetengeneza vifaa vya kujikinga (maski) na visafishio vya kitabibu, vinavyo hitajika kwa ajili ya kujilinda na virusi vya Korona.
Mkuu wa shirika hilo Ustadh Maitham Bahadeli amesema kua: “Tunapenda kuwaambia raia wa Iraq kua shirika letu ndani ya muda mfupi limefanikiwa kitengeneza maski na visafishio vya kitabibu vinavyoweza kutumiwa na raia wote wa Iraq, kutokana na mahitaji ya sasa kiafya ya kujilinda na virusi vya Korona, sambamba na kudhibiti mfumko wa bei.
Tambua kua shirika lilitangaza kuongeza utengenezaji wa maski na visafishio hivyo mara tano zaidi ya ilivyokua ikitengeneza awali, kwa ajili ya kugawa kwa wananchi na vituo vya afya katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine ili kujilinda na hatari ya virusi vya Korona.