Kuzaliwa kwa mlango wa haja (Baabul-Hawaaij) Abdullahi Radhwii (a.s).

Maoni katika picha
Imamu Hussein (a.s) alipata mtoto siku kama ya leo, mwezi tisa Rajabu na inasemekana ulikua mwezi kumi Rajabu mwaka wa (60h), mji wa Madina uling’ra kwa kuzaliwa kwake, mjukuu wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) walifurahi sana, kwa bwana wa vijana wa peponi kupata mtoto, waumini wakaanza kumuomba Mwenyezi Mungu kupitia utukufu wake, wakamfanya kuwa mlango wa kupitishia haja zao na kuzipeleka kwa Mwenyezi Mungu.

Baba yake: Imamu Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s) mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mama yake: Rubaab mtoto wa Imrii Qais mtoto wa Adi –Mshairi maarufu-.

Kupewa kwake jina: Baada ya kuzaliwa kwake (a.s) Imamu Hussein (a.s) alimpa jina la Ali Asghar, kama alivyo wapa majina watoto wake wengine ya Ali Akbar na Ali Sajjaad, alisema (a.s): (Hata kama Mwenyezi Mungu akinipa watoto elfu moja nitawapa jina la Ali), kutokana na mapenzi na ukarimu kwa baba yake mdhulumiwa wa kwanza duniani Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).

Mwanajeshi wa Karbala mwenye umri mdogo zaidi: Abdullahi Radhwii ni mwanajeshi mdogo zaidi wa Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala, na walii wa Mwenyezi Mungu mkubwa zaidi, pia ni mlango wa haja mbele ya Mwenyezi Mungu, na mdhulumiwa mkubwa sana katika historia, aliuwawa kishahidi akiwa ni mtoto wa miezi sita huku akiwa na kiu, kwa mkuki uliotiwa sumu wenye ncha tatu uliorushwa na maluuni Harmala bun Kaahil Asadi Kuufi mkuki huo ulimchinja kabisa, akiwa mikononi mwa baba yake katika vita ya Karbala, alizikwa na Imamu Zainul-Aabidina pembeni ya baba yake Imamu Hussein (a.s).

Ziara yake: Imetajwa na Imamu Hujjat (a.f) katika ziaratu Naahiya, pale aliposema: (Amani iwe juu ya Abdillahi bun Hussein, mtoto anaenyonya aliye pigwa mkuki na kuloana damu, ambae damu yake ilipaa angani, aliye chinjwa kwa mkuki akiwa mikonono mwa baba yake, Mwenyezi Mungu amlaani aliye muuwa Harmala bun Kaahil Asadii na mchinjaji wake).

Miongoni mwa kauli za washairi ni:

  • 1- Sayyid Haidari Hilliy anasema:

Kwa upole aliinama kumbusu mtoto wake *** mkuki ukambusu kabla yake na kumchinja.

Alizaliwa katika wakati mgumu *** na hatimae mkuki ukamlenga shingoni mwake.

  • 2- Shekh Muhammad Ridhwa anasema:

Lau ungemuona amebeba mtoto wake *** ungeona ni mwezi wa badri umebeba nuru yake.

Akiwa amelowa damu yake *** iliyotokana na mkuki uliompasua.

Utadhani mkuki upo shingoni kwake *** mwili wake ulikua unangáa kama dhahabu.

Alipolia na kupiga kelele bibi Laila *** akaita kwa sauti kubwaa.

Akasema Abdullahi anakosa gani *** hadi ashambuliwe kwa kuchomwa mkuki.

Nilikua nataraji watampa maji *** mambo hayakua kama nilivyokua nataraji.

Hawakumpa maji walipo ombwa *** hata tone moja la maji hawakutoa.

Najitolea kwa mtoto anayenyonya mdhulumiwa *** najitolea nafsi yangu kama naweza kua fidia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: