Kuahirishwa kwa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu-Shahada

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu-Shahada imetangaza kuahirishwa kwa kongamano hilo, ambalo lilitakiwa lifanyike mwanzoni mwa mwezi wa Shabani ujao (1441h).

Tamko liliyotolewa na kamati ya maandalizi ya kongamano hilo linasema kua: (Kutokana na mazingira yaliyopo katika taifa letu kwa sasa, uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya chini ya maelekezo ya viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba hizo umeamua kuahirisha kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu-Shahada la mwaka huu (1441h).. na badala yake kutakua na hafla za kawaida, za kusherehekea kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya katika mwezi mtukufu wa Shabani).

Kumbuka kua kongamano la Rabiu-Shahada huandaliwa na kugharamiwa kwa ukamilifu na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu lilipo anzishwa, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: