Baada ya kumaliza kazi ya kufunga taji kwenye dirisha la kaburi ya bibi Zainabu (a.s) nchini Sirya, lililotengenezwa katika kiwanda kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuzinduliwa siku mbili zilizo pita, mafundi walio simamia kazi hiyo walianza kulisafisha na kulitia manukato dirisha tukufu la Aqiilah bani Hashim (a.s).
Kazi hiyo ilihusisha kusafisha dirisha kwa vifaa maalum visivyo athiri madini yaliyo tumiwa katika kutengeneza dirisha hilo, na vinavyo lifanya liwe na muonekano mzuri kila mahala bila tofauti yoyote.
Baada ya kumaliza kazi ya usafi wakaweka manukato kama yale wanayo tumia katika dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kumbukuka kua dirisha hilo lilizinduliwa siku mbili zilizo pita, baada ya kumaliza kazi ya kulifunga iliyo fanywa na mafundi wa kitengo cha utengenezaji wa madirisha na milango ya makaburi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lililo sanifiwa na kutengenezwa na kitengo hicho, nayo ni kazi ya kwanza kufanywa kwa ajili ya malalo iliyopo nje ya Iraq.