Katika kumbukumbu ya (29): Tambua namna malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yalivyo shambuliwa katika maandamano ya Shaabaniyya

Maoni katika picha
Watu wa Karbala na mazuwaru wa malalo ya Abulfhadhil Abbasi (a.s) wanakumbuka shambulio la kinyama lililofanywa katika maandamano ya Shaabaniyya, wamefanya kumbukumbu ya (29) ya shambulio hilo, lililo fanyika mwezi wa Machi mwaka wa 1991m.

Miongoni mwa mambo yanayo fanywa na watu wa Karbala na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ni kujikumbusha namna zilivyo shambuliwa malalo mbili tukufu ndani ya siku 15 (Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya) pamoja na eneo la katikati ya haram mbili na sehemu zinazo zunguka eneo hilo, kutoka angani na ardhini bila heshima yeyote.

Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ilishambuliwa moja kwa moja na ikapata madhara makubwa kwenye kubba lake tukufu, ukuta wa uzio, mlango wa Kibla na saa pamoja na mnara wake, sambamba na jengo la haram na pambo la dhahabu huku milango mingine ya haram ikivunjika na kuwaka moto, jambo lililosababisha mipasuko mingi ndani na nje ya jengo la haram. Wanajeshi waliotekeleza unyama huo wakateka eneo lote la haram tukufu na wakakamata vijana wengi huku wengine wakiwapiga risasi, wakaiba vitu vingi vya malalo hiyo tukufu.

Watu wa Karbala wanasema kuwa; Utawala wa Sadam ulivamia mji wa Karbala, ukavunja nyumba za watu na ukashambulia haram ya Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s), hawakutosheka na unyama huo bali waliyalenga maeneo yote matakatifu na wakayashambulia kwa mabomu.

Kwa mujibu wa wafuatiliaji wa mambo wanasema kuwa, shambulio hilo lilikuwa ni muendelezo wa mashambulio kama hayo yaliyokuwa yameshafanywa mara nyingi na utawala wa Sadam.

Kumbuka kua uongozi wa kisheria ulirejea katika Ataba tukufu baada ya kuanguka kwa utawala wa Sadam, ndio baadhi ya wakazi wa Bagdad wakakabidhi kwa kitengo cha habari na utamaduni picha adimu ambazo hazikuwahi kuonyeshwa miaka ya nyuma, tumeziweka katika moja ya kurasa za picha kwenye mtandao wetu, ukitaka kuziona ingia katika link ifuatayo: https://alkafeel.net/photos/index.php?v=section&id=24
makamu rais wa wa kitengo tajwa Sayyid Aqiil Yasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Picha hizo ni za maandamano ya Sha’baniyya katika mji wa Karbala, zinaonyesha unyama uliofanywa na utawala wa Sadam katika mji wa Karbala na Ataba zake, na uharibifu uliofanyika pamoja na dharau iliyo onyeshwa na wafuasi wake, picha hizo zimesha onyeshwa kwenye maonyesho tofauti ndani na nje ya Iraq, ili kuonyesha ukatili uliofanywa na utawala wa Ba’thi chini ya Sadam ndani ya miaka (35) aliyo tawala Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: