Shirika la Khairul-Juud lawatahadharisha wateja wake: Ili kupata kinga inayotakiwa lazima kufuata maelekezo ya utumiaji

Maoni katika picha
Shirika la Khairul-Juud limesisitiza ulazima wa kufuata maelekezo ya namna ya kutumia vifaa vya kinga inavyo tengeneza ili kujikinga na virusi vya Korona.

Kuhusu swala hilo tumeongea na mkuu wa shirika Ustadh Maitham Bahadeli, amesema kuwa: “Vifaa vya kujikinga (maski) na visafishio vitakavyo ingizwa sokoni, vitaambatanishwa na maelekezo ya matumizi ambayo lazima yafuatwe, jambo hilo ni muhimu sana kwani linaambatana na afya pamoja na mazingira, kila mtumiaji lazima afuate maelekezo ya matumizi”.

Akaongeza kua: “Kila mtumiaji anatakiwa afuate maelekezo yaliyo andikwa kwenye kifaa anacho tumia na azingatie kiwango, haifai kupunguza wala kuongeza kiwango kilicho ainishwa, ukifuata maelekezo utapata matokeo mazuri na unaweza kupata matokeo mabaya kwa kuacha kufuata maelekezo”.

Tambua kuwa shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Khairul-Juud, lilitangaza kuwa limejiandaa kuzalisha vifaa vya kujikinga (maski) na visafishio mara tano zaidi ya uzalishaji wake wa kawaida, kwa ajili ya kugawa kwa wananchi na katika vituo vya afya vya Karbala na mikoa mingine, ili kujikinga na hatari ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: