Misafara ya misaada inayo andaliwa na idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya bado inaendelea kwenda kuwasaidia wapiganaji wa Hashdi Shaábi, msafara wa (Wanaotarajia rehema za Mwenyezi Mungu) kutoka mkoa wa Baabil umekwenda Swalahu Dini katika mji wa Matwibijah.
Mkuu wa msafara huo, Ustadh Sattaar Hussein Shiyaai amesema kua: “Huu ni moja ya misafara tuliyo fanya na tunayo endelea kufanya, jambo hili tumemuahidi Mwenyezi Mungu na Marjaa Dini mkuu, tutaendelea kuwasaidia ndugu zetu wanaojitolea kulinda taifa letu, hili ndio jambo dogo tunalo weza kufanya”.
Akaongeza kua: “Wanamsafara wamejitolea mali zao binafsi na kukusanya vikapu (vifurushi) vya chakula sambamba na kugawa chakula kilicho pikwa, hawakuishia kuwapa wapiganaji wa Hashdi Shaábi peke yake, bali waliwapa pia wanajeshi wa muungano waliokuwepo kwenye mji huo”.
Akasisitiza kua: “Pamoja na mazingira magumu ya mvua lakini tunaendelea kuwasaidia wapiganaji wa Hashdi Shaábi wanao hitajia misaada, tunajitahidi kuwapa kila tunacho weza miongoni mwa chakula na vitu vingine”.
Wapiganaji wameshukuru sana kwa kupewa misaada hiyo, na wamepongeza jitihada zinazo fanywa na idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuendelea kuwasaidia bila kuchoka.