Msimamo wa kisheria kuhusu virusi vya Korona na njia za kuondoa balaa hilo

Maoni katika picha
Miongoni mwa mihadhara inayo tolewa kila siku na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ni mihadhara ya kubainisha msimamo wa kisheria kuhusu virusi vya Korona na njia za kujikinga na hatari za madhara yake, pamoja na wajibu wa waumini kisheria kuhusu maradhi hayo.

Mihadhara hutolewa kila siku karibu na wakati wa swala ya Duhuraini chini ya uhadhiri wa masayyid na mashekhe wa kitengo cha Dini, na hubainisha msimamo wa kisheria, mihadhara ya siku za nyuma ilikua inahusu ubaya wa ufisadi pamoja na mada za kinga ni bora kuliko tiba, kama wanavyo sema madaktari.

Pia wameeleza hadithi ya Mtume (s.a.w.w) ya kukataza kuondoka au kuingia katika mji uliokumbwa na maradhi ya Tauni (hadithi hiyo inatumiwa kujihadhari na virusi vya Korona vilivyopo duniani kwa sasa) kutokana na madhara yanayo weza kupatikana kwa mgonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, ili kuhakikisha maradhi hayasambai kwenye miji mingine.

Pia wamehimiza ulazima wa kujilinda kama alivyo amrisha Mwenyezi Mungu mtukufu, chini ya kanuni isemayo “Kuondoa madhara yanayo tarajiwa” na ulazima wa kufuata maelekezo ya madaktari, mambo hayo pia yamesisitizwa na Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya Ijumaa ya mwisho, na kuacha kudharau au kupuuza ugonjwa huu.

Katika mihadhara hiyo huzungumziwa mambo ya kifiqhi na kiaqida pia, yanayo endana na mazingira halisi ya jamii, sambamba na kuwahimiza waumini wasiache kumtegemea Mwenyezi Mungu na kufanya subira katika hukumu zake, humaliza kwa kujibu maswali ya mazuwaru kwa wazi kwa ajili ya faida kwa wote.

Kumbuka kua kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesha jibu swali walilokua wakijiuliza wairaq wengu na ulimwengu wa kiislamu kwa ujumla, lisemalo: Je tunayopitia ni mtihani wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake au ni nini? Akajibu kupitia mada isemayo: (Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kwa ajili ya kuondoa balaa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: