Atabatu Abbasiyya tukufu inafuatilia kwa karibu hali ya majeruhi na kufanya mchakato wa kusafarisha wahanga hao katika nchi ya Sirya

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amelipa umuhimu mkubwa tukio la ajali iliyo tokea pembezoni mwa mji wa Damaskas nchini Sirya, sambamba na kufanya mchakato wa kusafirisha miili ya watu walikufa kwenye ajali hiyo.

Makomu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Ustadh Maitham Zaidi amesema kua: “Mara tu baada ya kusikia habari hii, Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amelipa umuhimu mkubwa swala la kufuatilia hali ya afya ya majeruhi na mchakato wa kusafirisha miili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo”.

Akaongeza kua: “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya waliopo Sirya kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha bibi Zainabu (a.s) wanafanya mchakato rasmi wa kuwasafirisha majeruhi na wahanga wa ajali hiyo kwa kushirikiana na ubalozi wa Iraq”.

Akabainisha kua: “Sisi kwa upande wetu kama uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu tumewasiliana na ofisi ya waziri mkuu na muungano wa opresheni za kijeshi pamoja na wizara ya ulinzi kwa ajili ya kuandaa ndege ya kivita itakayo safirisha majeruhi na miili ya walikufa kwenye ajali hiyo, kwa kushirikiana pia na serikali ya mkoa wa Karbala, tumekamilisha maandalizi yote yanayo hitajika”.

Akasisitiza kua: “Kazi ya kusafirisha maiti na baadhi ya majeruhi itafanywa leo kwa msaada wa Mwenyezi Mungu”.

Kumbuka kua ajali imetokea jana pembezoni mwa mji wa Damaskas nchini Sirya, kati ya basi zilizokua zimebeba mazuwaru wa kiiraq na gari la kubeba mafuta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: