Jua la uongofu limechomoza yaipasa dunia ijae furaha, kwa nini isiwe hivyo wakati ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa pambo la Dini na kiongozi wa waumini, mbora wa wachamungu Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).
Kutokana na kumbukumbu hiyo pamoja na utaratibu wa Atabatu Abbasiyya katika kuadhimsha siku kama hizi za matukio ya furaha, haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imepambwa na kuwekwa mabango yenye jumbe mbalimbali zinazo ashiria furaha, sambamba na kuwashwa taa za rangi ambazo huwashwa katika matukio ya furaha.
Korida za haram zimewekwa mabango yaliyo andikwa baadhi ya sifa za pekee alizokuanazo kiongozi wa waumini (a.s), pamoja na kuweka miti ya mauwa kwenye milango ya haram na nje ya uzio wa haram.