Maoni katika picha
Akaongeza kua: “Kuna watumishi wa Atabatu Abbasiyya waliopo Sirya wanafuatilia hatua zote za usafirishaji wa maiti na hali za majeruhi, kuna mawasiliano ya hali ya juu kwa ajili ya kuondoa vikwazo vyote na kuhakikisha majeruhi wanapata huduma za lazima kimatibabu”.
Akabainisha kua: “Hili sio jambo jipya kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, imesha wahi kugharamia matibabu ya majeruhi wa tukio la kigaidi lililo walenga mazuwaru nchini Sirya, pamoja na kusafirisha mashahidi walio uwawa kwenye tukio hilo, japokua kulikua na mazingura magumu wakati huo”.
Katika tamko la kwanza lililotolewa na naibu katibu mkuu Ustadh Maitham Zaidi alisema kua: “Hakika uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu tumewasiliana na ofisi ya waziri mkuu na muungano wa opresheni za kijeshi pamoja na wizara ya ulinzi kwa ajili ya kuandaa ndege ya kivita itakayo safirisha majeruhi na miili ya walikufa kwenye ajali hiyo, kwa kushirikiana pia na serikali ya mkoa wa Karbala, tumekamilisha maandalizi yote yanayo hitajika”.