Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza safari ya anga kwenda kusafirisha maiti za watu walikufa kwenye ajali iliyotokea nchini Sirya

Maoni katika picha
Jioni ya Jumapili ndege ya kivita chini ya wizara ya ulinzi ya Iraq, ikiwa na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya pamoja na wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala na jopo la madaktari, ilianza safari kwenda Sirya kubeba majeruhi na miili ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) walikufa kwenye ajali.

Tambua kua uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umekua ukifuatilia kwa karibu hali za majeruhi na mchakato wa kuwasafirisha kwa kushirikiana na ubalozi wa Iraq nchini Sirya, pamoja na kufanya mawasiliano na waziri mkuu na muungano wa opresheni za kijeshi sambamba na wizara ya ulinzi, kwa ajili ya kupata ndege ya kivita itakayo beba maiti na majeruhi wa ajali hiyo, na tayali mahitaji yote ya lazima yamekamilika.

Tambua kua ujumbe wa Atabatu Abbasiyya uliwasiri Sirya Alfajiri ya leo (12 Rajabu 1441h) sawa na (8 Machi 2020m) kuangalia hali ya majeruhi na kuwatia moyo kuhusu usalama wao, wamekamilisha mchakato wa vibali vya vifo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: