Kuzaliwa kwa simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s)

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo –mwezi kumi na tatu Rajabu miaka thelathini baada ya mwaka wa tembo- dunia ilinawirika kwa kuzaliwa bwana wa mawasii na kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Alizaliwa ndani ya Alkaaba tukufu, haikuwahi kutokea kabla yake wala baada yake kuzaliwa mtu ndani ya nyumba hiyo tukufu ya Mwenyezi Mungu, hakika ilikua ni heshima kubwa kwake kuzaliwa ndani ya nyumba hiyo.

Mama yake alimzaa ndani ya haram ya Mwenyezi Mungu na msikiti

Akiwa mweupe mtakasifu msafi wa nguo mzawa mwema.

Imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kuhusu kuzaliwa kwake, anasema: (Abbasi bun Abdulmutwalib na Yazidi bun Qaánab walikua wamekaa baina ya kundi la bani Hashim na kundi la Abdul-Iuza pembezoni mwa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, akaja Fatuma bint Asadi bun Hashim mama wa kiongozi wa waumini (a.s) akiwa na ujauzito (mimba) ya kiongozi wa waumini yenye miezi tisa, akasema: akasimama pembeni ya nyuma tukufu, akiwa na uchungu, akanyanyua mikono yake juu na akasema: Ewe Mola mimi nakuamini na ninaamini waliyo kuja nayo mitume kutoka kwako, naamini mitume wako wote na vitabu vyako vyote, ninasadikisha maneno ya babu yangu Ibrahim, na yeye ndiye aliyejenga nyumba hii, nakuomba kwa haki ya nyumba hii na aliye ijenga, na kwa haki ya kiumbe huyu aliye tumboni mwangu, ambaye hunizungumzisha na kuniliwaza, na mimi naamini kua yeye ni moja ya alama zako, nifanyie wepesi kujifungua kwangu.

Abbasi bun Abdulmutwalib na Yazid bun Qaánab wakasema: Baada ya kuomba dua hiyo Fatuma bint Asadi, tuliona nyumba ikipasuka na fatuma akaingia na kutoweka machoni kwetu, kisha nyumba ikarudi kama ilivyo kua kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, tukataka kufungua mlango ili baadhi ya wanawake waingie wakamsaidie katika kujifungua lakini mlango haukufunguka, tukajua kua huo ni muujiza wa Mwenyezi Mungu mtukufu, Fatuma akabakia ndani ya nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu, ilipofika siku ya tatu nyumba ikapasuka palepale ilipo pasuka mara ya kwanza na Fatuma akatoka akiwa na Ali (a.s) mikononi mwake, halafu akasema: Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ameniteua katika viumbe wake, na kanifanya kua bora kushinda alio wateua kabla yangu, Mwenyezi Mungu mtukufu alimteua Asia bint Muzahimu hakika yeye alimuabudu kwa siri sehemu ambayo mtu akimuabudu Mwenyezi Mungu anateswa, na Maryam bint Imrani Mwenyezi Mungu alimteua na akamfanya amzae Issa (a.s), akatikisha mti wa mtende zikadondoka tende zilizo wiva vizuri.

Hakika Mwenyezi Mungu ameniteua mimi na kunifanya kua bora zaidi yao na juu ya wanawake wote waliotangulia kabla yao, kwa sababu mimi nimejifungua ndani ya nyumba yake, na nimekaa humo siku tatu nakula matunda ya peponi, nilipo taka kutoka nikiwa na mtoto wangu mikononi nilisikia sauti ikiniambia: Ewe Fatuma mpe jina la (Ali) mtoto huyo, hakika mimi ni Aliyyul-Aála, na mimi nimemuumba kwa uwezo wangu na utukufu wangu na uadilifu wangu na jina lake nimelitoa katika jina langu, nimemfundisha adabu zangu na nimempa amri yangu, na nimemfungulia elimu yangu, na amezaliwa ndani ya nyumba yangu, naye atakua mtu wa kwanza kuadhini katika nyumba yangu, na kuvunja masanamu na kuyatupa, ataniheshimu na kunitukuza, naye ni Imamu baada ya kipenzi wangu na Mtume wangu Muhammad (s.a.w.w), na niwasii wake, amefaulu atakae mpenda na kumnusuru, na ameangamia atakae muasi na kumdharau).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: