Hospitali ya rufaa Alkafeel imepokea majeruhi wa ajali iliyotokea Sirya

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel imepokea majeruhi wa ajali iliyotokea Sirya pembezoni mwa mji wa Damaskas ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) wa kiiraq, baada ya kuwabeba kwa kutumia gari za wagonjwa kutoka uwanja wa ndege wa Najafu hadi hospitalini hapo.

Hospitali ilikua imesha jiandaa kwa mapokezi hayo, mara tu baada ya kuwasili waliingizwa kwenye gari za wagonjwa na huduma za awali zikaanza moja kwa moja ili kubaini namna ya kuwagawa kulingana na hali ya kila mgonjwa, na kuendelea na matibabu.

Serikali ya mkoa wa Karbala na idara ya afya pamoja na idara ya uwanja wa ndege wa Najafu walikua na mawasiliano ya hali ya juu pamoja na ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha majeruhi wanafikishwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel haraka iwezekanavyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: