Kuwasiri katika hospitali ya Alkafeel: Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatembelea majeruhi wa Sirya na kutaka wapewe huduma bora zaidi

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu unao husisha wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo umetembelea hospitali ya rufaa Alkafeel kuangalia hali ya majeruhi wa ajali ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) iliyotokea pembezoni ya mji mkuu wa Sirya Damaskas, baada ya kuwasiri katika hospitali hiyo asubuhi ya leo kupitia uwanja wa ndege wa Najafu.

Mmoja wa wajumbe waliotembelea hospitali ya rufaa Alkafeel ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kufuatia maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ya kugharamia matibabu ya majeruhi wote wa ajili ya mazuwaru iliyo tokea Sirya, sawa majeruhi huyo anatibiwa ndani au nje ya Iraq, sambamba na kufuatilia kwa karibu mchakato wa kusafirisha majeruhi na miili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo, baada ya majeruhi kufika katika horpitali ya Alkafeel, tumeunda kamati itakayo fuatilia hali za majeruhi na kuwatia moyo kuhusu afya zao, pamoja na kuwafikishia salamu na dua za watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) za kuwaombea wapone haraka”.

Akabainisha kua: “Hakika madaktari wa hospitali ya Alkafeel wanafanya kila wawezalo kwa ajili ya kuwapa huduma bora zaidi za kimatibabu na kuhakikisha wanapata kila kinacho hitajika”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: