Atabatu Abbasiyya imetoa tamko kuhusu kusafirishwa majeruhi wa ajali ya Sirya

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa tamko kuhusu kusafirishwa majeruhi wa ajali ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) iliyotokea Sirya pembezoni mwa mji mkuu wa Damaskas.

Tamko hilo limetolewa kwenye kikao na waandishi wa habari leo mwezi (13 Rajabu 1441h) sawa na (9 Machi 2020m) asubuhi, ndani ya ukumbi wa mikutano katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limetolewa na Dokta Mushtaqu Abbasi Muan kwa niaba ya rais wa kitengo cha habari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Atabatu Abbasiyya tukufu inatangaza kua imefanikiwa kusafirisha maruwaru wa kiiraq waliopata ajali pembezoni mwa mji mkuu wa Sirya Damaskas, wamewasiri leo asubuhi (13 Rajabu 1441h) sawa na (9 Machi 2020m).

Jumla ya majeruhi walio wasili ni thelathini, tumewagawa katika mikoa mitatu (Bagdad, Muthanna na Karbala) kuna ambao wanamajeraha madoge, wenye majeraha ya saizi ya kazi na wenye majeraha makubwa.

Kuna majehuhi wengine wanne ambao madaktari wameshauri waendelee kutibiwa katika hospitali za Sirya, kwa sababu hali zao za kiafya haziruhusu kuwasahirisha kwa sasa.

Atabatu Abbasiyya tukufu inawaombea majeruhi wote wapone haraka, na inawapa mole wahanga wote na kuziomba familia zao kuwa na subira, na inatoa shukrani rasmi kwa kila aliyeshiriki katika mchakato huu, hususan wafuatao:

  • - Waziri mkuu wa Iraq/ idara ya matukio.
  • - Wizara ya afya ya Iraq na idara ya afya ya mkoa wa Karbala.
  • - Wizara ya ulinzi.
  • - Wizara ya mambo ya nje.
  • - Uongozi wa umoja wa opresheni za kijeshi.
  • - Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Karbala.
  • - Ubalozi wa Iraq nchini Sirya.
  • - Idara ya uwanja wa ndege wa Najafu.
  • - Serekali ya Sirya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: