Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu utaanza kusafirisha maiti za watu waliokufa kwenye ajali nchini Sirya kwa anga

Maoni katika picha
Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeanza hatua ya pili ya jukumu la kusafirisha miili ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) waliokufa kwenye ajali nchini Sirya, hatua hii inakuja baada ya kuwapeleka majeruhi katika hospitali ya Alkafeel na kupata matumaini ya afya zao.

Kwa mujibu wa maelezo ya kaimu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Ustadh Maitham Zaidi, amesema: “Wamesafirishwa kwa anga baada ya kuwasiliana na wizara ya mambo ya nje ya Iraq pamoja na ubalozi wa Iraq nchini Sirya, na wizara ya ulinzi ya Iraq na uongozi wa muungano wa opresheni za kijeshi sambamba na serikali ya mkoa wa Karbala, kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa miili ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) waliokufa kwenye ajili”.

Akaendelea kusema: “Kuna mchakato ulikua umesha fanywa na wajumbe wa Atabatu Abbasiyya waliopo katika mji mkuu wa Sirya, ikiwa ni pamoja na kupata vibali vya vifo na kuandaa usafiri wa kubeba maiti kutoka hospitali hadi uwanja wa ndege”.

Akasisitiza kua: “Maiti hizo zitasafirishwa kwa ndege ya kijeshi ya Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: