Muhimu: Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu unakwenda Damaskas kwa anga kuchukua miili ya watu waliokufa kwenye ajali nchini Sirya

Maoni katika picha
Jeoni ya leo ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeanza safari kuelekea mji mkuu wa Sirya Damaskas kuchukua miili ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) wa kiiraq waliokufa kwenye ajali iliyo tokea pembezoni mwa mji wa Damaskas, kazi ya kusafirisha miili hiyo itaanza mapema kesho Jumanne kwa kutumia ndege ya kivita ya Iraq.

Mchakato wa kuwasafirisha umefanywa kwa kushirikiana kati ya wizara ya mambo ya nje ya Iraq na ubalozi wa Iraq nchini Sirya pamoja na wizara ya ulinzi ya Iraq na uongozi wa umoja wa opresheni za kijeshi sambamba na serikali ya mkoa wa Karbala na idara ya afya ya mkoa huo.

Tambua kua maandalizi yote yamekalika katika mji mkuu wa Sirya Damaskas chini ya ufuatiliaji wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya uliopo huko, ikiwa ni pamoja na kuandaa vibali vya vifo na usafiri wa kuwatoa hospitalini hadi uwanja wa ndege.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: