Muhimu: Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umekamilisha vibali vya watu waliokufa kwenye ajali nchini Sirya na mchakato wa kuwapeleka uwanja wa ndege unaendelea

Maoni katika picha
Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliopo mji mkuu wa Sirya Damaskas umekamilisha vibali vya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) wa kiiraq waliokufa kwenye ajali iliyo tokea pembezoni mwa mji wa Damaskas.

Tayali wamesha andaa usafiri wa kuwatoa hospitalini hadi uwanja wa ndege baada ya kuwafanyia ibada ya kuwashindikiza katika malalo ya bibi Zainabu (a.s).

Tambua kua mchakato wa kuwasafirisha umefanywa kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje ya Iraq na ubalozi wa Iraq nchini Sirya pamoja na wizara ya ulinzi ya Iraq na uongozi wa muungano wa opresheni za kijeshi sambamba na serikali ya mkoa wa Karbala na idara ya afya ya mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: