Maoni katika picha
Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulikwenda kwa anga (9 Machi 2020) katika mji mkuu wa Sirya Damaskas kushughulikia mchakato wa kusafirisha wahanga wa ajali iliyotokea pembezoni mwa mji wa Damaskas Sirya.
Mchakato huo umefanywa kwa kushirikiana na wizara ya nje ya Iraq pamoja na ubalozi wa Iraq nchini Sirya, na wizara ya ulinzi ya Iraq na uongozi wa muungano wa opresheni za kijeshi sambamba na serikali ya mkoa wa Karbala na idara ya afya ya mkoa huo.
Tambua kua maandalizi yote yamekamilika katika mji mkuu wa Sirya Damaskas chini ya ufuatiliaji wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya uliopo huko, ikiwa ni pamoja na vibali vya vifo na usafiri wa kuwatoa hospitali na kuwapeleka uwanja wa ndege.