Asubuhi ya leo Jumanne ya mwezi (14 Rajabu 1441h) sawa na (10 Machi 2020m) misafara mikubwa ya kushindikiza mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) waliokufa kwenye ajali nchini Sirya imeanza, baada ya Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na sekta mbalimbali kusafirisha miili hiyo kutoka Damaskas kwa ndege ya kivita ya Iraq hadi katika uwanja wa ndege wa Najafu.
Misafara ya kuwashindikiza imeanzia barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kushiriki wakazi wengi wa Karbala na watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala na vyombo vya ulinzi na usalama.
Atabatu Abbasiyya imeandaa kila kitu kwa ajili ya shughuli hii, na imetenga sehemu ndani ya haram tukufu kwa ajili ya swala ya jeneza na ziara, baada ya ibada hiyo msafara utaelekea katika haram ya Imamu Hussein (a.s) ukipitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu kisha watapelekwa katika makazi yao ya mwisho.
Kumbuka kua miili hiyo ilifika kwenye uwanja wa ndege wa Najafu leo Alfajiri chini ya usimamizi wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya baada ya kufanya ibada ya kuishindikiza katika malalo takatifu ya bibi Zainabu (a.s), pamoja na kusimamia mchakato wote wa safari kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje ya Iraq na ubalozi wa Iraq nchini Sirya, na wizara ya ulinzi ya Iraq pamoja na uongozi wa muungano wa opresheni za kijeshi sambamba na serikali ya mkoa wa Karbala na idara ya afya ya mkoa huo.