Kwaheri ya mwisho: Watu wa Karbala wanashindikiza mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) waliokufa kwenye ajali nchini Sirya

Maoni katika picha
Watu wa Karbala asubuhi ya Jumanne (14 Rajabu 1441h) sawa na (10 Machi 2020m) wamewashindikiza wairaqi waliokwenda kumzuru bibi Zainabu (a.s) nchini Sirya na kufariki kwenye ajali ya kusikitisha.

Umati mkubwa wa watu umejitokeza kuwashindikiza pamoja na watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wakiwemo wawakilishi wa serikali ya Karbala na vyombo vya ulinzi na usalama bila kuzisahau familia za wahanga wa ajali hiyo, misafara ya washindikizaji ilianzia katika barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye haram yake takatifu, ambapo imesomwa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na ziara ya Imamu Ridhwa (a.s) na ziara ya Imamu Hujjat Imamu wa zama (a.f) na kaswida za kuomboleza za Husseiniyya.

Baada ya hapo wakazungushwa katika Kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha wakaenda kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) kwa kupitia katikati ya uwanja wa haram mbili tukufu, na kufanyiwa kama walivyo fanyiwa katika malalo ya ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Baada ya kumaliza ibada hizo walipelekwa katika makazi yao ya mwisho kwa kutumia gari zilizo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua maiti ziliwasili uwanja wa ndege wa Najafu leo Alfajiri chini ya usimamizi wa Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na baada ya kufanyiwa ibada ya kushindikizwa katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), sambamba na kusimamia mchakato mzima wa kuwasafirisha kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje ya Iraq pamoja na ubalozi wa Iraq nchini Sirya, na wizara ya ulinzi ya Iraq na uongozi wa muungano wa opresheni za kijeshi sambamba na serikali ya mkoa wa Karbala na idara ya afya ya mkoa huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: