Mafundi wa idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya wameanza kushona maski kwa ajili ya kupunguza pengo la vifaa hivyo katika taifa na kwenye vituo vya afya, kutokana na kuhitajika kwa wingi vifaa hivyo, kwa ajili ya kujikinda na virusi vya Korona, awamu ya kwanza wameshona zaidi ya maski (10,000), zitagawiwa bure kwa mazuwaru na watumishi wa malalo takatifu pamoja na makundi mengine ya watu.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Ustadh Abduzuhura Daud Salmaan, amesema kua: “Ni Imani ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuunganisha nguvu katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, imechukua hatua mbalimbali katika kupambana na maambukizi ya virusi hivyo, kwa ajili ya kuwalinda mazuwaru na watumishi, hivi karibuni tumeamuriwa kushona maski kutokana na kuanza kukosekana vifaa hivyo katika soko, kutokana na ukubwa wa mahitaji, hiyo ndio sababu ya sisi kuanza kufanya kazi hii”.
Akabainisha kua: “Awamu ya kwanza tumeshona zaidi ya maski (10,000), tutazigawa kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya na hospitali ya rufaa Alkafeel pamoja na kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), awamu zingine tutagawa kwa makundi mengine ya watu”.
Akamalizia kwa kusema: “Vitambaa tunavyo tumia vimefanyiwa vipimo na kupasishwa na kamati ya afya ya wataalam kutoka idara ya afya ya mkoa wa Karbala, tunashona kwa kufuata maelekezo na vipimo vya kidaktari”.