Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani amejibu swali lililotumwa katika ofisi yake kuhusu kushiriki swala ya jamaa kwenye mazingira ya kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Korona.
Swali linasema: Ni upi mtazamo wa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu kuhusu kushiriki swala ya jamaa katika siku hizi ambazo tunashuhudia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Korona?
Jibu: kutokana na kuwepo kwa katazo la mikusanyiko kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, ni wajibu kuliheshimu na kulifanyia kazi.