Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya utakwenda katika malalo ya Aqiilah Twalibina bibi Zainabu binti Ali (a.s), kuhuisha kumbukumbu ya kifo chake katika mji mkuu wa Sirya Damaskas siku ya kesho Jumatano (15 Rajabu 1441h) sawa na (11 Machi 2020m).
Rais wa ujumbe huo bwana Nizaar Ghina Zubaidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa majonzi na huzuni kubwa kufuatia kauli ya bibi Zainabu (a.s) isemayo: (Fanya vitimbi vyako na ongeza juhudi yako, namuapa Mwenyezi Mungu hutafuta utajo wetu), na chini ya utaratibu endelevu wa Atabatu Abbasiyya katika kukumbuka misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na dhulma walizo fanyiwa, ujumbe wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) utaelekea katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) kwa ajili ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo chake (a.s).
Akaongeza kua: “Tayali yamewekwa mapambo meusi ndani ya haram ya Zainabiyya, na kufanywa majlisi ya kuomboleza iliyo hutumiwa na Mheshimiwa Shekh Swahibu Twaiy, sambamba na kugawa chakula kwa mazuwaru na watumishi wengine kwa kushirikiana na watumishi wa malalo hiyo takatifu”.
Tambua kua imeandaliwa ratiba maalum katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuhuisha msiba huu.