Asubuhi ya leo mwezi (15 Rajabu 1441h) sawa na (11 Machi 2020m) Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimetoa tamko la kusitisha swala za jamaa kutokana na maelekezo ya kujilinda yaliyo tolewa na idara ya afya ya mkoa wa Karbala kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru watukufu.
Kumbuka kua Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani jana alijibu swali lililotumwa kwenye ofisi yake kuhusu hukumu ya kushiriki swala ya jamaa katika mazingira ya kusambaa maambukizi ya virusi vya Korona.
Swali lilikua linasema: Ni upi mtazamo wa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu kuhusu kushiriki swala ya jamaa katika siku hizi ambazo tunashuhudia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Korona?
Jibu: kutokana na kuwepo kwa katazo la mikusanyiko kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, ni wajibu kuliheshimu na kulifanyia kazi.