Kituo cha wahadhiri kimepata cheti cha utawala bora Izu (9001:2015 ISO)

Maoni katika picha
Kituo cha wahadhiri chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimepewa cheti cha utawala bora, baada ya kufuata kanuni za kimataifa Izu (9001:2015 ISO) za misingi ya utawala bora, sambamba na misingi sahihi ya maendeleo endelevu.

Mkuu wa kituo Mhandisi Jafari Hussein Qutbu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kupata cheti cha kimataifa cha utawala bora ni ushahidi kua kituo cha wahadhiri kinafanya kazi kwa kufuata misingi ya kielimu katika sekta zete, ikiwa ni pamoja na kufuata masharti yote ya utawala bora sambamba na kuzalisha bidhaa zenye ubora mkubwa unaokubalika kimataifa”.

Akaongeza kua: “Kutokana na juhudi ya kitengo cha miradi ya kihandisi na msaada ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kituo cha wahadhiri kinafanya kazi vizuri na kwa mpangilio unaokubalika na viwango vya kimataifa, aidha kinatoa huduma bora kwenye sekta zote, kituo cha wahadhiri wa kihandisi ni mhimili mkubwa wa miradi yote ya kihandisi na kipimo cha mafanikio ya miradi hiyo”.

Kumbuka kua mradi wa kituo cha wahadhiri kwenye sekta ya tofali unategemewa na miradi yote ya ujenzi wa nyumba katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: