Kitengo cha habari na utamaduni kimetoa kitabu mashuhuri zaidi katika mji wa Najafu

Maoni katika picha
Kituo cha upigaji picha nakala kale na faharasi katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya kimetoa kitabu cha, (faharasi ya nakala kale ya maktaba ya Ayatullah Sayyid Jafari na mwanae Allamah Sayyid Hashim Aali Bahrul-Uluum) juzu la kwanza.

Kitabu hicho chenye juzu (150) kina mada (289), maudhui za kitabu hicho ni; tafsiri, hadithi, aqida, fiqhi, usulu, lugha, adabu, nasabu, tiba na zinginezo.

Maktaba ya Sayyid Jafari na mwanae ni mashuhuri zaidi katika mji wa Najafu, historia yake inajulikana, inahazina kubwa ya vitabu adimu, kunakaribu vitabu (550).

Tambua kua maktaba hiyo tukufu ilihamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya kulinda isipotee, kutokana na yaliyojiri hapa Iraq miongoni mwa fitina na matukio ya kuumiza, hadi ikatengewa sehemu na maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa usalama wake, kwa lengo la kuilinda na kuitengenezea faharasi hadi itakapo andaliwa sehemu yake ramsi katika mji wa Najafu, tayali imekamilika faharasi yake iliyo andaliwa na kituo cha upigaji picha nakala kale na faharasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: