Mawakibu Husseiniyya zimepanda miche ya mitende (1000) katika barabara ya (Yaa Hussein)

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan amesema kua, wawakilishi wa kitengo hicho katika mkoa wa Diyala (ofisi ya Jidaidah-Shatu) wamepanda miti katika barabara ambayo hutumiwa na mazuwaru wengi (Yaa Hussein) inayo onganisha kati ya Najafu na Karbala.

Akaongeza kua: “Zimeshiriki mawakibu nyingi na wahudumu wa Husseiniyya katika mji wa Jidaidah-Shatu pamoja na idadi kubwa ya watu waliojitolea misaada mbalimbali kwa watoa huduma”.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Abbasi Makiy amesema kua: “Wakazi wa mji huu kupitia mawakibu Husseiniyya wamejitolea zaidi ya miche (1000) ya mitende kwa ajili ya kupandwa katika barabara ya (Yaa Hussein – Yaa Ali) inayo onganisha kati ya Najafu na Karbala, miche hiyo imetolewa na mawakibu Husseiniyya kwa kushirikiana na wakazi wa mji huo, baada ya kuwasiliana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya”.

Akasema: “Watu wanaojitolea tumewagawa sehemu mbili; sehemu ya kwanza ni wale ambao wamejitolea miche kutoka kwenye mashamba yao na kuikusanya sehemu moja, na sehemu ya pili ni wale waliobeba miche hiyo na kwenda kuipanda kwenye barabara tajwa”.

Akasema kua: “Tumepata mbegu za aina tofauti, kuna: (Barhi, Zuhudi, Khastawi, Barbun, Makawi), miti itapendezesha barabara hiyo inayotumiwa zaidi na mazuwaru watembea kwa miguu sambamba na kuboresha mazingira”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: