Tolea la kumi na tatu la jarila la (turathi za Hilla)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha toleo la kumi na tatu (13) la jarida la (turathi za Hilla), linalo elezea turathi za Hilla, toleo hilo limepasishwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu.

Limejaa tafiti na hakiki zenye umuhimu mkubwa kwa turathi za Hilla, tafiti zake zimejikita katika mada kuu tatu:

Mada ya kwanza: tafiti mbili katika tarjama, nazo ni: (mazungumzo ya kifalsafa kati ya Allamah Hilliy na mhakiki Nasru Dini Tusi) na (Risala Sa’diyya ujumbe wa muundo na madhumuni).

Mada ya pili: tafiti mbili katika mambo ya sekula kuhusu historia ya utamaduni wa wanachuoni wa Hilla, nazo ni: (swala la kielimu kati ya Nasru-Dini Tusi na wanachuoni wa Hilla) na (hauza za kielimu za Hilla katika vitabu vya wanachuoni wa Iran.. utafiti katika kuanza kwake na sifa zake kielimu)

Mada ya tatu: utafiti katika lugha, adabu na maarifa ya Quráni, miongoni mwake ni: (mabadiliko ya sauti katika lahaja ya kiarabu cha wakazi wa mji wa Hilla) na (masahihisho ya kilugha ya Dokta Ali Jawadi Twaahir) na mengineyo.

Tambua kua jarida la turathi za Hilla ni moja ya majarida yanayo tolewa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, linategemewa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, pia linausajili wa kimataifa, na lilipewa tuzo na Daru Kutubu Wal-Wathaaiq Iraaqiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: