Maelezo muhimu ya kukarabati msahafu adim ambao historia yake inarudi karne ya sita hijiriyya

Maoni katika picha
Ofisi ya kukarabati nakala kale chini ya maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya imetoa maelezo muhimu kuhusu ukarabati wa msahafu adimu ambao historia yake inarudi karne ya sita hijiriyya, baada ya kupita miaka mingi na kutelekezwa kwa muda mrefu kuliko sababisha kuharibika kurasa za msahafu huo, umefanyiwa marekebisho kwa njia ya kisasa zaidi.

Ustadh Lithi Lutufi mkuu wa kituo hicho amesema kua: “Historia ya msahafu huu inarudi mwishoni mwa karne ya sita hijiriyya, umeandikwa kwa hati ya kale, majina ya sura yameandikwa kwa zafarani na maandishi mengine yameandikwa kwa wino wa Karubuni, pembezoni mwa maandishi kuna mapambo ya mimea, vitu hivyo vimeufanya kua adimu”.

Akaongeza kua: “Tulipo anza kufanya upembuzi kamili wa kutanbua uharibifu uliokua umetokea kwenye msahafu huo, tulibaini yafuatayo:

  • - Karatasi hazikua kamaili, kuna upungufu wa karatasi na maandishi.
  • - Karatasi zilikua zimepasuka.
  • - Jarida lilikua limepasuka na kuharibika maandishi yake.
  • - Kulikua na vipande vya karatasi ambavyo havirekebishiki.
  • - Kuandaa idadi kubwa ya karatasi na kuziambatanisha na zingine katika kufanya marekebisho.

Akaongeza kua: “Baada ya kumaliza upembuzi tukaanza ukarabati, tumefanya juhudi kubwa kuuweka katika muonekano mzuri, kwa rehema za Mwenyezi Mungu na baraka za mwenye malalo pamoja na weledi wa mafundi tumefanikiwa kufanya ukarabati na kuondoa dosari zote, miongoni mwa tuliyofanya ni kuondoa uchafu na vumbi kwa tukumia vifaa maalum, pamoja na kuziba sehemu zilizo pasuka kwa kutumia karatasi maalum za Japani na gundi, baada ya kuteneza karatasi zikashonwa pampja kwa kutumia uzi wa katani, halafu tukaanza kutengeneza jalada kwa kutumia ngozi asilia, kisha tukatengeneza mfuko wa kitambaa kwa ajili ya kuuweka kwenye kifungashio cha Ataba tukufu”.

Akamaliza kwa kusema: “Msahafu umekarabatiwa kwa kutumia njia za kisasa zaidi, tumerekebisha mapungufu yote bila kuathiri hati yake ya zamani, pamoja na kulinda umbo lake asilia, kazi imekamilika ndani ya muda uliopangwa, sambamba na kutengeneza nakala maalum ya kwenye Kompyuta kwa ajili ya kulinda uhalisia wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: