Idara ya ustawi wa jamii imeanza opresheni ya kujikinga na virusi vya Korona

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kazi ya kujikinga na virusi vya Korona, kupitia ofisi zake za mikoani kwa kuwajengea uwelewa raia kuhusu virusi vya korona sambamba na kupuliza dawa sehemu za umma zinazo tumiwa na wananchi.

Kazi hiyo imeanzi kaskazini ya Baabil, kiongozi wa opresheni hiyo Ustadh Qasim Ma’muri amesema kua: “Katika kufanyia kazi maelekezo ya umma kuhusu kujikinga na virusi vya Korona, tumewaagiza watumishi wetu kupuliza dawa sehemu zote za umma na kugawa vifaa vya kujikinga na maangukizi ya virusi vya Korona kwa askari wote waliopo kwenye vituo vya ukaguzi”.

Huku idara ya ustawi wa jamii katika mkoa wa Muthanna ikiendelea na harakati zake ilizo anza toka siku ya kwanza kutangazwa hatari ya virusi hivyo na kupatikana mgonjwa wa kwanza, ambapo wanasambaza vipeperushi vinavyo elezea hatari ya virusi kwa Korona na namna ya kujikinga navyo, na jambo la pili wanapuliza dawa sehemu za umma na kwenye makazi ya watu, walianzia katika wilaya ya Khadhar kwa kupuliza dawa sokoni na kwenye nyumba za makazi ya watu katika mji wa Imamu Hussein (a.s) na bado wanaendelea hadi vitongoji vyote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: