Wapi utakapo shuhudia vipande vya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kushambuliwa kwake?

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala-kale katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetenga sehemu maalum ndani ya ukumbi wake kwa ajili ya kuonyesha mabaki ya vipande vya kubba baada ya kushambuliwa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa vifaru wakati wa maandamano ya Shaabaniyya, ambayo tupo katika siku za kumbukumbu ya maandamano hayo, na kuangazia tukio hilo la kusikitisha.

Ustadh Swadiq Laazim rais wa kitengo cha makumbusho ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Historia inamatukio mengi, kuna mambo hubaki katika akili kwa miaka mingi bila kufutika, likiwemo tukio la maandamano ya Sha’baniyya, na kushambuliwa kwa Ataba za Karbala katika maandamano hayo, yaliyo fanyika mwaka (1991m), tukio ambalo tupo katika siku za kumbukumbu yake, la kushambuliwa kwa vifaru na mabomu kuliko pelekea kuuwawa na kujeruhiwa watu wengi ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ikiwa ni pamoja na kuharibika kubba, saa, mlango wa Kibla pamoja na sehemu zingine za haram”.

Akaongeza kua: “Fikra ya kutenga sehemu maalum ya kuonyesha hatua muhimu za kushambuliwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu inatunza kumbukumbu halizi ya matukio hayo, likiwemo tukio hili baya, imetengenezwa sehemu yenye ukubwa wa (mt 4.5 x 2) na kuwekwa kila kitu kilichotokana na shambulio hilo, miongoni mwa vitu hivyo ni:

  • - Vipande vya dhahabu vya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) vilivyo toka baada ya kushambuliwa kubba hilo kwa vifaru, vinavyo onyesha athari ya shambulio hilo.
  • - Vipande vya ukuta wa haram tukifu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Vipande vya mmoja wa milango ya haram tukufu.
  • - Bendera ya Kubba tukufu yenye ishara za kuungua na kushambuliwa kwa kifaru”.

Akabainisha kua: “Sehemu hiyo pamewekwa screen (tv) kwa ajili ya kuweka vipande vya video vinavyo onyesha tukio hilo na kuelezea uharibifu uliofanyika, sambamba na kuelezea kila kitu kilichopo sehemu hiyo kwa kiarabu na kiengereza”.

Kumbuka kua mauwaji na vitisho dhidi ya mazuwaru wa Ataba za Karbala pamoja na kushambuliwa majengo ya Ataba hizo na sehemu takatifu ilikua ni desturi ya watawala wote waovu (matwaghuti) katika kila zama tangu kutokea kwa mauwaji ya Twafu Muharam kumi mwaka wa (61h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: