Katika kushajihisha ubunifu: Kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu amempa zawadi mwanafunzi aliye gundua kosa la kielimu katika kitabu cha Tashriih

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amempa zawadi mwanafunzi wa mwaka wa pili katika kitivo cha udaktari/ chuo kikuu cha Al-Ameed bi Ghadiir Nizaar Dhiyaau, aliyegundua kosa la kielimu katika kitabu cha Tashriih (Elsevier) kilicho sambazwa na Daaru Nashri ya kimataifa (Gray’s Anatomy).

Sayyid Swafi amesema kua: “Taifa hujengwa na watu wake, mwanafunzi huyu na wenzake wanategemewa na taifa, daima sisi tunaheshimu uwezo wa mtu na tunaihusia familia yake iongeze juhudi ili kumuwezesha kufikia malengo yake, na kumjengea moyo na kujiamini zaidi”.

Akamuambia kua: “Daima mwanadamu haoni makosa na wala hajali, lazima tuwe na malengo ili tuweze kufanya kazi, kila hatua anayopitia mwanadamu inachangamoto, kuna njia ya kushinda changamoto, unatakiwa kuwa na malengo na ufanye kazi ya kufanikisha malengo yako, kwa kutumia njia sahihi na kubaini makosa”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu akuwezeshe kulitumikia taifa lako, uwajali watu na kuwatumikia kwa nguvu zako zote, hakika wanahitaji huduma yako, uonyeshe kwa vitendo elimu yako ya chuo, elimu yenye faida ni ile inayonufaisha watu, jiepushe na kiburi wala usisahau familia yako iliyosaidia mafanikio yako pamoja na walimu waliotumia muda wao kukufundisha”.

Naye bi Ghariir amefurahi sana kupewa zawadi hiyo, akasema kua siku ya leo haitafutika katika akili yake na itaendelea kumhamasisha zaidi katika masomo yake.

Rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali akasema kua: “Sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu au kiongozi wake mkuu wa kisheria kutoa zawadi kama hizi, historia yake imejaa matukio kama haya ya kushajihisha akili na kusaidia vipaji vya wanafunzi wa kiiraq, zawadi hii ni sehemu ndogo katika zawadi nyingi ambazo zimesha tolewa, zenye mchango mkubwa kwa wanafunzi wote kwa ujimla”.

Zawadi hizi zinafungua mlango wa kuwatia moyo wanafunzi wa kiiraq na kuwajengea kuamini uwezo wao wa kujenga taifa lao, ndio jambo linalo sisitizwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: