Kikosi maalum cha kupambana na virusi vya Korona kimezishukuru Ataba mbili tukufu kwa msaada wao

Maoni katika picha
Kikosi maalum cha kupambana na virusi vya Korona katika mkoa wa Karbala, kimeshukuru na kupongeza kazi zinazofanywa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa kuwasaidia kuzuwia maambukizi ya Korona.

Yamesemwa hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa leo asubuhi katika majengo ya ofisi za mkoa wa Karbala, na kutangaza hatari ya kutembea katika mitaa yote ya Karbala kwa muda wa siku tatu kuanzia Jumatatu, kwa lengo la kuendelea kupuliza dawa katika majengo yote ya serikali na eneo la katikati ya mji na barabara zake sambamba na ofisi mbalimbali.

Kikosi hicho kimetoa wito kwa wakazi wote wa Karbala watoe ushirikiano kwa watu wa afya na vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na kufuata maelekezo yao, kwa ajili ya usalama wao na familia zao kutokana na hatari ya Korona.

Atabatu Abbasiyya inaendelea kuchukua tahadhari mbalimbali za kujilinda na virusi vya Korona, na kufanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idaza ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: