Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi kimeanza hatua ya pili ya opresheni ya kupuliza dawa kwenye barabara za mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa opresheni ya kuzuwia kusambaa kwa virusi vya Korona, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kwa kushirikiana na shirika la Khairul-Juud, kimeanza hatua ya pili ya kupuliza dawa katika mitaa ya Karbala, baada ya kumaliza hatua ya kwanza hapo jana.

Hatua hii ni sehemu ya mkakati mkubwa wa upuliziaji wa dawa unaotekelezwa na kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya Korona katika mkoa wa Karbala, ulio anza asubuhi ya leo Jumatatu (16 Machi 2020m) na utafanyika kwa siku tatu.

Ustadh Maitham Zaidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Opresheni hii ni sehemu ya mkakati wa kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, kikosi cha Abbasi kimeshiriki kwenye opresheni ya kupuliza dawa barabara zote za Karbala chini ya ratiba iliyopangwa na kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusu vya Korona”.

Akasisitiza kua: “Kazi hii ni sehemu ya kazi zitakazo endelea kufanywa na kikosi cha Abbasi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala, chini ya maombi ya serikali ya mkoa”.

Akabainisha kua: “Kazi zetu haziishii kwenye kupuliza dawa peke yake, bali tunawafundisha wananchi namna ya kutambua dalili za maambukizi ya virusi vya Korona na njia za kujikinga na maambukizi hayo pamoja na kuwagawia maski”.

Kumbuka kua kikosi kilianza tangu jana kupuliza dawa angani, ikiwa na hatua ya kwanza ya kutumia ndege zisizokua na rubani, ambapo walipuliza maeneo yanayo zunguka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: