Kuendelea kupuliza dawa katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Kikosi cha kupambana na majanga katika Atabatu Abbasiyya, kimeanza kazi ya kupuliza dawa katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kulinda usalama wa watumishi na mazuwaru sambamba na wakazi wa maeneo hayo.

Tumeongea na kiongozi wa kikosi cha mambo ya kitabibu katika Ataba tukufu Dokta Osama Abdulhassan amesema kua: “Kazi ya kupuliza dawa katika eneo la katikati ya harama mbili tukufu ni sehemu ya ratiba ya Atabatu Abbasiyya inayo husisha mji mkongwe na maeneo yanayo zunguka malalo mbili tukufu, tunapuliza dawa kutoka katika shirika la Khairul-Juud kwa kufuata maelekezo ya wizara ya afya ya Iraq”.

Msimamizi wa utendaji wa kazi hiyo, Ustadh Hassan Ali Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kikosi cha kupambana na maambukizi ya Korona chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi, kimechukua jukumu la kupuliza dawa mji mkongwe kwa kufuata ratiba maalum, ambapo mji wameugawa sehemu tofauti na leo wameanza kupuliza dawa maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya na sehemu za kutawadhia, masanduku ya kutunzia vitu (amanaati), sehemu za kuvulia viatu pamoja na ukuta wa nje wa Ataba tukufu, kazi inaendelea hadi tutakapo kaliza jukumu tulilopewa”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha chukua hatua mbalimbali za kujiknga na maambukizi ya virusi vya Korona, aidha inafanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na wizara ya afya, sawa maelekezo hayo yawe yanahusu Ataba tukufu, mji mkongwe au mkoa wote kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: