Kikosi cha Abbasi: Tunafanya kila tuwezalo kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na tunatoa wito kwa raia watoe ushirikiano kwa kujikinga na kulinda usalama wao

Maoni katika picha
Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (Liwaau 26 Hashdi Shaábi) kinafanya kila kiwezalo katika kuisaidia serikali na wizara ya afya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kinawaomba wananchi watoe ushirikiano kwa kujilinda na kufuata maelekezo yanayo tolewa na taasisi za afya kwa ajili ya kulinda usalama wao.

Taarifa inasema kua kikosi kinafanya kila kiwezalo kwa kushirikiana na serikali katika kupuliza dawa kwenye mji tofauti hapa mchini, kimewaita wapiganaji wake elfu moja wa hakiba kwa ajili ya kupambana na usambaaji wa virusi vya Korona, tayali wamesha piga hatua kubwa katika kupuliza dawa sehemu za umma, mitaani, sehemu za mikusanyiko ya watu na sehemu zingine muhimu, wataendelea na kazi hiyo hadi hatari ya Korona itakapo isha kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Aidha kikosi kinatoa elimu kuhusu virusi vya Korona na namna ya kujikinga navyo kwa kusambaza vipeperushi vilivyo jaa maelekezo ya kidaktari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: