Marjaa Dini mkuu amesisitiza ulazima wa serikali kuwapatia wahudumu wa afya vifaa vyote muhimu katika kujikinga na hatari ya maambukizi ya virusi vya Korona, akasema hakuna udhuru unaokubalika wa kutowapa vifaa hivyo.
Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani la swali lililotumwa ofisini kwake, kuhusu hatari ya maambukizi waliyo nayo madaktari, wauguzi na wasaidizi katika hospitali na vituo vya afya wanapo wahudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona, ifuatayo ni nakala ya jibu hilo:
(Serikali inatakiwa iwape vifaa vyote vinavyo hitajika kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona, wala haitakiwi kutoa udhuru katika hilo).