Marjaa Dini mkuu amesema kua; kazi inayo fanywa na madaktari, wauguzi na wengineo ya kuwatibu na kuwahudumia watu wenye maambuizi ya virusi vya Korona, umuhimu wake ni sawa na wapiganaji waliopo kwenye uwanja wa vita kwa ajili ya kulinda taifa lao na raia.
Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani la swali lililotumwa ofisini kwake, kuhusu hatari ya maambukizi waliyo nayo madaktari, wauguzi na wasaidizi katika hospitali na vituo vya afya wanapo wahudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona, ifuatayo ni nakala ya jibu hilo:
(Bila shaka wanacho fanya ndugu zetu –pamoja na changamoto- ni kazi kubwa isiyokua na mfano, umuhimu wake unafana na wapiganaji waliopo kwenye uwanja wa vita kulinda taifa na raia wake).