Marjaa Dini mkuu amesema kua juhudi zinazo fanywa na wahudumu wa afya katika kupambana na virusi vya Korona Mwenyezi Mungu ameibariki, atakaejitolea uhai wake katika njia hiyo atapata thawabu za shahidi.
Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani la swali lililotumwa ofisini kwake, kuhusu hatari ya maambukizi waliyo nayo madaktari, wauguzi na wasaidizi katika hospitali na vituo vya afya wanapo wahudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona, ifuatayo ni nakala ya jibu hilo:
(Bila shaka Mwenyezi Mungu mtukufu anaona juhudi zao hapa duniani na atawalipa kesho akhera, bali atakaejitolea uhai wake katika njia hiyo atapata thawabu za shahidi siku ya hesabu).