Kikosi cha Abbasi na jeshi la wananchi wanaendesha opresheni kubwa ya kupuliza dawa mji wa Karbala sambamba na tangazo la kutotembea barabarani.

Maoni katika picha
Jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala pamoja na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi), wanaendesha opresheni kubwa ya kupuliza dawa pamoja na kutoa elimu kuhusu njia za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, baada ya kuanza kutekelezwa amri ya kuacha kutembea.

Kiongozi wa jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala Kapteni Twahiri Hamiid amesema kua: “Kutokana na ratiba ya kamati maalum ya kupambana na Korona, na baada ya kuanza kutekelezwa amri ya kutotembea, tumeanza kupuliza dawa kwenye barabara zote, chochoro na viwanja vya wazi, kuanzia nje ya hadi katikati ya mji”.

Akasema: “Makundi tofauti yameshiriki katika kazi hii, lakini kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kina nafasi maalum katika kulinda usalama wa raia”.

Kiongozi wa madaktari wa kikosi cha Abbasi Ustadh Swalehe Janabi amesema kua: “Baada ya maelekezo ya viongozi wa kikosi cha Abbasi, tumeunda kamati na kuandaa dawa pamoja na vifaa, tunapuliza dawa nyumba baada ya nyumba, pamoja na kutoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona kwa kugawa vipeperushi na kubandika mabango yaliyo andaliwa na kikosi hivi karibuni”.

Wananchi wamepongeza kazi zinazo fanywa na kikosi cha Abbasi na wameahidi kutoa ushirikiano, wameonyesha umuhimu wa kazi hii katika kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona, wakasema kua sio jambo jipya kwa kikosi cha Hashdi Shaábi kusimama pamoja na wananchi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: