Mihadhara ya kujenga uwelewa kuhusu virusi vya Korona na mambo yanayo hitajika kwa wafanyakazi

Maoni katika picha
Miongoni mwa mambo yaliyofanywa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, idara ya madaktari chini ya kauli mbiu isemayo (kinga ni bora kuliko tiba) na kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo himiza kuchukua tahadhari ya maradhi haya.

Idara imeandaa ratiba ya kutoa mihadhara ya kuzungumzia virusi hivyo, imeanza na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuwajengea maarifa zaidi kuhusu virusi vya Korona, sambamba na kuwajulisha hatari ya virusi hivyo na njia za maambukizi yake pamoja na namna ya kujikinga, na kuwapa vifaa vya kujikinda kwa ajili ya usalama wao na mazuwaru watukufu.

Watumishi wa vitengo tofauti katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamehudhuria mihadhara hiyo kama ilivyo pangwa katika ratiba, pamoja na kuwapa kipaombele watumishi wenye muingiliano wa moja kwa moja na mazuwaru au wanaofanya kazi katika maeneo yanayo zunguka Ataba.

Vimetambulishwa virusi vya Korona na chanzo chake, pamoja na namna vinavyo hama kutoka sehemu moja hadi nyingine na muda vinao ishi pamoja na madhara yake, wahadhiri wameeleza njia mbalimbali za kufanya baada ya kuambukizwa virusi hivyo –Allah atuepushie-, na jambo kubwa ni kufuata maelekezo ya madaktari na kutumia vifaa vya kujikinga.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: