Uzinduzi wa kituo cha utafiti wa kielimu (maabara).

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeweka msingi wa kuanzishwa kituo cha utafiti wa kielimu (maabara), itakayo jikita katika tafiti za afya, kilimo na mambo mengine.

Kwa mujibu wa rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali amesema kua: “Mradi huu ni sehemu ya harakati za chuo katika kuboresha sekta ya elimu, hususan katika mambo yanayo husu taifa la Iraq, ukizingatia kua ni mbegu ya kwanza ya mustakbali wa tafiti za kielimu”.

Akasisitiza kua: “Kutokana na kuanzishwa kwa maktaba hii, kunatusukuma kutafuta na kuandaa wataalamu wa ki-Iraq, na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya tafiti zao na kuzifanyia kazi kwa faida ya baadae”.

Akaongeza kua: “Hakika maabara hii itaweka mazingira maruri, lengo la kuanzishwa kwake ni kuboresha utafiti, na kushirikiana kufanya kazi kwa maslahi ya taifa letu kipenzi”.

Maabara inavipimo tofauti vya kielimu, miongoni mwa vipimo hivyo ni: (kemia kwa ujumla, kemia ya uhai, dawa na sumu, viumbe hai na visivyo hai, urutumishaji wa nyukilia, kitengo cha wanyama), kitakua na vifaa vya kisasa vinavyo endana na utafiti wa kila kitu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: