Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kuchukua hatua za kujikinga

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kuchukua hatua za kujikinga na virusi vya Korona, chini ya usimamizi na maelekezo ya kamati maalum ya kujikinga na virusi vya Korona katika Ataba tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya idara ya maktaba, hatua hizo zinafanywa na kituo cha ukarabati wa nakalakale chini ya usimamizi wa kitengo cha kemia, baada ya kupewa semina ya namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, tahadhari wanayo chukua inaendana na mazingira ya maktaba.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha chukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kazi hiyo, pamoja na kufanyia kazi maelekezo yote yanayo tolewa na idara za afya ndani ya Ataba, katika vitengo vyake na katika mji mkongwe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: